KIBURI CHA PENDO

 

Emakulata Msafiri

Pendo alikuwa msichana mzuri na mwenye akili kijijini Mlimba lakini alikuwa na kiburi kingi. Alimdharau kila kijana wa kawaida hasa Baraka aliyempenda kwa dhati ambaye alikua anafanya kazi ya seremala.

Siku moja Baraka alijaribu kumuonesha hisia zake kwa barua. Pendo alimjibu kwa dharau:

“Mimi siwezi kutoka na seremala Tafadhali usinipotezee muda.”

Miaka ikapita. Pendo akaenda mjini akafuata maisha ya starehe. Lakini maisha yakamgeuka. Alirudi kijijini akiwa maskini na mpweke.

Aliporudi alimkuta Baraka ni tajiri mwenye familia yenye furaha.Pendo alihisi majuto makubwa. Alimwendea Baraka na kuomba msamaha.

Baraka alimjibu kwa upole: “Nilikupenda kwa moyo wangu wote lakini sasa nimejifunza kupenda wale wanaonithamini.”

Pendo alibaki akitazama machozi yakimtiririka. Kiburi chake kilikuwa kimemnyang’anya pendo la kweli.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments