JINSI MTOTO ANAVYOWEZA KUSHIRKIANA NA WENGINE

 

Emakulata Msafiri

Mtoto ni kiumbe anayekua na kujifunza kila siku kupitia mazingira yanayomzunguka. Moja ya tabia muhimu anayopaswa kujifunza ni kushirikiana na wengine. Kushirikiana ni tendo la kufanya mambo kwa pamoja na kuishi kwa upendo. Watoto wanapojifunza kushirikiana wakiwa bado wadogo wnakua kuwa watu wenye maadili mema na wenye mchango chanya katika jamii.

Mtoto anaweza kushirikiana na wengine kwa kucheza pamoja. Michezo ni sehemu muhimu ya maisha ya mtoto. Anapocheza na wenzake hujifunza namna ya kugawana vitu kama mipira, kucheza kwa zamu na kuheshimu hisia za wengine. Kupitia michezo mtoto hujenga urafiiki na hujifunza kuwasiliana na wenzake kwa heshima.

Vilevile mtoto anaweza kushirikiana kwa kugawana vitu na wenzake. Kwa mfano anapogundua kuwa rafiki hana kalamu au chakula anaweza kumpa chake kidogo. Tendo hili humjenga kuwa na moyo wa huruma, upendo na ukarimu. Kugawana ni ishara ya mshikamano na huimarisha urafiki kati ya watoto.

Aidha kushirikiana hujumuisha kusikiliza na kuheshimu maoni ya wengine. Mtoto anapojifunza kuwa si kila wakati yeye ndiye mwenye hoja sahihibhuanza kuthamini fikra za wengine. Hii humsaidia kushirikiana vizuri katika mijadala au maamuzi ya kikundi bila ubinafsi.

Mtoto anayejifunza kushirikiana hujijengea tabia nzuri ambazo humsaidia katika maisha ya sasa na ya baadaye. Huweza kuishi kwa amani na wenzake, kujenga urafiki wa kweli na kuwa mtu mwema katika jamii.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments