Emakulata Msafiri
Kuendesha gari kunahitaji umakini mkubwa uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka na uelewa wa alama za usalama. Watoto hawana sifa hizi hivyo wanaweza kusababisha ajali kwa urahisi. Ajali hizo zinaweza kusababisha majeraha makubwa au hata vifo.
Lakini pia sheria za nchi nyingi ikiwemo za Tanzania zinakataza watu wa chini ya umri wa miaka 18 kuendesha gari. Hii ni kwa sababu wanaotunga sheria wanatambua hatari inayoweza kujitokeza ikiwa watoto wataendesha magari.
Hata hivyo kuna baadhi ya watu wanaodai kuwa mtoto anaweza kuendesha gari iwapo anafundishwa na mzazi wake kwa lengo la kumwandaa kwa maisha ya baadaye. Ingawa nia inaweza kuwa nzuri bado si sahihi kwa sababu sheria haimruhusu mtoto kuendesha gari bila kuwa na leseni halali.
Naweza kusema kwamba watoto kuendesha gari sio jambo jema wala salama. Ni hatari kwa mtoto mwenyewe wa familia yake na kwa jamii kwa ujumla. Ni jukumu la kila mzazi, mlezi na mwanajamii kuhakikisha kuwa watoto hawaruhusiwi kuendesha magari mpaka wafikie umri unaotakiwa na kupata mafunzo rasmi. Hii itasaidia kupunguza ajali kulinda maisha na kuendeleza kizazi kinachoheshimu sheria na taratibu za nchi.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment