Emakulata Msafiri
Katika maisha ya kila siku wazazi wana nafasi ya kipekee na muhimu sana katika malezi na makuzi ya mtoto. Mtoto anapata ujuzi mwingi kutoka kwa wazazi wake hasa katika hatua za awali za maisha yake. Wazazi ni walimu wa kwanza kwa mtoto na ujuzi anaoupata kutoka kwao humsaidia katika maisha yake ya baadaye.
Mtoto hujifunza ujenzi wa lugha na mawasiliano kutoka kwa wazazi wake kupitia kuongea nao mtoto huanza kutambua maneno kuelewa maana yake na kuyatumia katika mazungumzo. Kwa mfano mtoto anapofundishwa kusema “asante” au “samahani” anaanza kujifunza mawasiliano ya kistaarabu yanayokubalika katika jamii.
Mtoto hufundishwa tabia na maadili mema kama vile uaminifu, heshima, unyenyekevu na kuwajali wengine. Wazazi humwelekeza mtoto kutofautisha kati ya jambo jema na baya. Kwa mfano wanamfundisha kutokudanganya kutoiba na kuwa mkarimu kwa wengine. Maadili haya humjenga mtoto kuwa mtu mwema na anayekubalika katika jamii.
Mtoto hujifunza ujuzi wa maisha ya kila siku kutoka kwa wazazi. Hii ni pamoja na kazi ndogondogo kama kufagia, kuosha vyombo, kupika au kupanga vitu. Kwa kumshirikisha mtoto katika shughuli hizi wazazi humwezesha kupata maarifa ya kujitegemea baadaye maishani.
NI wazi kuwa wazazi wana mchango mkubwa sana katika kumfundisha mtoto ujuzi mbalimbali muhimu katika maisha. Kupitia malezi yao ya kila siku mtoto hujifunza mambo mengi yatakayomsaidia kujitegemea kuheshimika na kuwa mwanajamii mwema. Kwa hivyo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment