Emakulata Msafiri
Juma alikuwa kijana wa miaka 14 mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mlimani. Alikuwa mtoto mtiifu, mchangamfu na mwenye bidii darasani. Wazazi wake walimfundisha kuwa na heshima kuogopa Mungu na kuepuka marafiki wabaya.
Siku moja baada ya shule marafiki zake watatu Dogo, Pato na Zaga walimvuta pembeni na kumwambia:
“Juma twende nyuma ya maduka kuna mtu anatupa hela tukimpelekea mzigo wake. Ni kazi rahisi halafu tutanunua chipsi na soda.”
Juma aliuliza “Mzigo gani?”
Wakamjibu “Usijali! Ni pakiti tu lakini ukifungua utaona unga mweupe… ni dawa ya kulevya lakini sisi hatutumii tunapeleka tu.”
Juma alishtuka. Aliwatazama na kusema kwa msimamo:
“Hapana! Sitaki kuhusika na jambo baya. Hela si kila kitu. Sina haja ya pesa haramu.”
Walimcheka na kumuita "mtoto wa mama" lakini Juma aliondoka. Alipofika nyumbani alimweleza mama yake kila kitu. Mama yake alimpongeza kwa ujasiri na kumuombea.
Baada ya wiki moja wale wavulana walikamatwa na polisi wakiwa na dawa hizo. Walifukuzwa shule na wazazi wao waliumia sana.
Juma alisifiwa na walimu na hata mkuu wa wilaya alikuja kumpa zawadi kwa uadilifu wake. Aliendelea kuwa mfano bora kwa watoto wenzake
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment