Emakulata Msafiri
Kuliku na bundi mmoja mzee. Alikuwa akiishi juu ya mti. Bundi alikuwa mtulivu hapendi makelele na kila usiku alitoka kutafuta chakula.
Wanyama wengine walimwona bundi kama wa ajabu kwasababu alikua anapenda kukaa kimya na mara nyingi walikua wenzake walikua wanamuuliza.
"Kwa nini huwa kimya sana?" wengine wakaongezea.
Lakini bundi hakupenda kujibu maswali mengi. Alijua wakati wake wa kusema unakuja.
Siku moja kulizuka ugomvi mkubwa kati ya wanyama nyani, fisi, pundamilia na wengine. Kila mmoja alitaka kuwa kiongozi wa msitu. Wakawa wanagombana kila siku bila suluhisho.
Simba mfalme wa msitu alikuwa amezeeka na akawaita wote kwa mkutano. "Nahitaji mnyama mwenye hekima atusaidie kupata suluhu."Wanyama wakakumbuka: "Bundi!"
Bundi akaitwa Kwa sauti ya upole alisema,
"Kiongozi si yule anayepiga kelele zaidi au aliye na nguvu zaidi bali yule anayesikiliza anayejali na mwenye maono kwa wote."
Wanyama wakatulia. Waliona hekima katika maneno ya bundi. Wakakubaliana kuchagua kiongozi kwa kupiga kura badala ya ugomvi.
Tangu siku hiyo wnyama walimheshimu bundi kama mzee mwenye hekima.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment