Emakulata Msafiri
Siku moja katika kijiji kidogo alIshi panya mdogo aliyependa sana kula chakula cha watu. Kila usiku aliingia jikoni na kula mchele, mahindi na vipande vya mkate vilivyobaki.
Lakini kulikuwa na tatizo moja jogoo mkubwa aliyeishi uani alikuwa mkali sana. Alikuwa kila wakati akimfukuza kipanya na kupiga kelele kubwa. Kipanya hakupenda kabisa kelele za jogoo.
Akaamua kupanga njama. Akasema“Nitafanya kitu ili jogoo huyu asiweze tena kunifukuza!”
Usiku mmoja panya aliiba pilipili nyingi na kuziweka kwenye chakula cha jogoo. Asubuhi jogoo alipokula chakula kile alianza kupiga chafya na hakuweza kupiga kelele kama kawaida.
Kipanya alifurahi sana:"Sasa nitakula kwa amani!"
Lakini usiku ulipofika, paka aliyezoea kuogopa kelele za jogoo alikuja kimya kimya. Jogoo hakuwa na sauti ya kupiga kelele kumwonya mtu yeyote.
Panya alipokuwa anakula jikoni paka alimtokea ghafla… na karibu amkamate! Panya alikimbia kwa shida sana
Kesho yake alikwenda kwa jogoo na kumwomba msamaha."Samahani rafiki yangu. Nilifikiri unanikwaza, kumb ulikuwa unaniokoa."
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment