CHURA NA CHEMCHEMI MPYA


Emakulata Msafiri

 Kulikuwa na kijiji kidogo ambacho kilikuwa na tatizo kubwa la maji. Watu walitembea umbali mrefu kwenda mtoni kila siku na mara nyingi walichoka sana. Watoto walichelewa shule kwa sababu walihitajika kusaidia kubeba maji.

 Kijiji hicho aliishi chura mdogo aliyeitwa Chugu. Chugu alikuwa tofauti na vyura wengine hakupenda kuona watu wakiteseka. Kila siku alipowaona watoto wakibeba ndoo nzito za majibmoyo wake ulihuzunika.

Siku moja Chugu alifikiri “Lazima nifanye jambo la kuwasaidia watu hawa. Mungu alinipa miguu ya kuruka na sauti ya kuimba labda naweza kutumia uwezo wangu kwa wema.”

Akaanza safari ya kwenda mtoni. Alifika na kuzungumza na maji kwa wimbo wake wa kipekee:

Maji yakasikia sauti ya Chugu. Kwa furaha na heshima maji yakaanza kutiririka yakifuata njia aliyopiga kwa miguu yake. Chugu alirukaruka kutoka mtoni mpaka kijijini akiacha njia ya maji nyuma yake.

Siku moja tu maji yalifika kijijini! Watu walishangaa sana walipoona chemchemi mpya ikitiririka karibu na nyumba zao. Walicheza, waliimba na walimshukuru sana Chugu.

Maji yale yakaendelea kutiririka na watoto wakaanza kwenda shule bila kuchoka. Wazee walipata maji karibu na kila mtu akajua kuwa mdogo huweza kufanya jambo kubwa.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments