Emakulata Msafiri
Watoto ni sehemu muhimu sana ya jamii yoyote ile. Wao ni msingi wa taifa la baadaye, na maendeleo ya nchi yoyote yanategemea jinsi watoto wake wanavyolelewa na kulindwa. Hata hivyo pmoja na umuhimu wao, watoto wengi hukumbana na changamoto mbalimbali ambazo huathiri ustawi wao wa kimwili, kiakili, kijamii na kihisia.
Unyanyasaji wa Watoto, Moja ya changamoto kubwa kwa watoto ni unyanyasaji. Watoto wengi hupitia mateso ya kimwili, kingono na kihisia. Baadhi ya wazazi au walezi huwapiga kupita kiasi, kuwatukana au kuwatumia kwa njia zisizofaa kama kazi za suluba au biashara ya ngono. Unyanyasaji huu huacha athari kubwa kwa mtoto ikiwa ni pamoja na hofu, msongo wa mawazo na hata kupoteza mwelekeo wa maisha.
Ukosefu wa Elimu Bora ,Watoto wengi hasa kutoka familia maskini hawapati fursa ya kwenda shule au hupata elimu duni isiyokidhi mahitaji ya sasa. Kukosa elimu hupelekea watoto wengi kuendelea kuwa katika mzunguko wa umasikini na kukosa ujuzi wa kujiendeleza baadaye.
Ukosefu wa Huduma za Afya,Watoto wengi hasa vijijini hawapati huduma bora za afya. Wanakosa chanjo muhimu matibabu ya haraka wanapougua na elimu ya afya. Hii husababisha vifo vya watoto wachanga na magonjwa ya mara kwa mara ambayo yangeweza kuzuilika.
Watoto wanahitaji ulinzi, upendo, elimu na mazingira salama ili waweze kukua na kuwa raia wenye mchango chanya katika jamii. Ni jukumu la kila mtu wazazi, serikali, walimu, mashirika na jamii kwa ujumla kuhakikisha kuwa changamoto hizi zinatatuliwa. Kuwekeza kwa mtoto ni kuwekeza kwa taifa zima.
emakulatemsafiri@gmal.com
0653903872



Post a Comment