BINTI WA MFALME JASIRI

Emakulata Msafiri

Zamani sana katika ufalme wa Kolelo alitawala mfalme mwenye busara aitwaye Mfalme Chambi. Alikuwa na binti mmoja tu Binti Nasya ambaye alilelewa kama kifalme lakini moyo wake haukupenda anasa alipenda kupigana kwa upanga, kupanda farasi, na kulinda watu wake.

Siku moja donda kubwa la ukame likaupiga mji mzima. Mito ikakauka mashamba yakafa na watu wakaanza kuhama. Wachawi wa mlimani wakampelekea mfalme ujumbe:

 “Mali zenu zote zitanusurika iwapo mtatoa sadaka ya dhahabu na kumtuma binti mfalme afanye ibada kwenye pango letu la siri.”

Mfalme Chambi akasitasita lakini Nasya akasimama mbele ya baraza na kusema kwa sauti kuu:

“Baba sitaki watu wetu wafe. Nitakwenda mwenyewe si kwa uoga bali kama shujaa wa kuokoa ufalme wetu.”

Usiku ule ule Binti Nasya alipanda farasi wake mweupe akaelekea kwenye milima ya wachawi. Alipofika pangoni wachawi waliamuru awekwe kifungoni hadi alfajiri.

Lakini usiku huo alichora ramani ya kutoka kwenye sanduku la wachawi akavunja minyororo yake kwa kipande cha jiwe kisha akachukua fimbo ya uchawi iliyokuwa ikilinda mvua.

Alipokuwa akikimbia, wachawi wakamfukuza kwa radi na moto. Nasya akapanda juu ya mwamba akapiga kelele:

“Msitu na maji ni zawadi ya Mungu si mali ya wachawi!”

Akapiga fimbo chini mara mawingu yakakusanyika mvua kubwa ikaanza kunyesha mito ikafurika tena.

Wachawi wakashangazwa na nguvu yake wakaanguka chini na kutawanyika.

Binti Nasya akarudi nyumbani akiwa amechafuka kwa matope lakini akitabasamu. Watu wote wakampokea kwa vigelegele na kumpa jina jipya

“Nasya Shujaa wa Mvua.”Kutoka siku hiyo mfalme alianzisha shule ya mashujaa kwa wasichana, akisema.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments