BINTI MWENYE MOYO WA DHAHABU

 

Emakulata Msafiri

 kulikuwa na msichana mmoja aitwaye Neema. Alikuwa anaishi na mama yake katika chumba kidogo cha kupanga. Ingawa hawakuwa na mali nyingi Neema alikuwa maarufu kwa kitu kimoja moyo wake wa dhahabu.

Neema alikuwa mwanafunzi wa sekondari na kila alipomaliza masomo alikwenda kwenye kituo cha watoto yatima kuwasaidia kufanya kazi zao za shule. Wakati mwingine aliwashonea nguo zao zilizoraruka au kuwaletea sabuni na penseli alizoweka akiba ya hela ya chakula chake.

Majirani walimshangaa. Walimwambia:

“Neema kwa nini unawasaidia sana watu wengine wakati wewe mwenyewe huna vya kutosha?”

Lakini Neema alijibu kwa upole:

“Maisha si kuwa na vingi Bali kutumia kidogo ulicho nacho kwa upendo.”

Siku moja mfanyabiashara mkubwa wa jiji hilo alipita kwenye kituo cha watoto yatima akiwa amejificha kama mtu wa kawaida kutafuta mtu wa kumsaidia kuongoza taasisi yake ya misaada. Aliona jinsi Neema alivyojali watoto alivyochangamka na alivyojitolea kwa moyo wote.

Miezi miwili baadaye Neema alipokea barua kutoka kampuni kubwa. Alialikwa kwenye usaili wa kazi na hakuwahi hata kuomba! Alipofika alikuta yule mfanyabiashara ambaye alimkumbuka kutoka kituoni.

Mfanyabiashara akasema:

“Niliona moyo wako wa dhahabu. Ndiyo sababu nataka uwe kiongozi wa mradi wetu wa kusaidia jamii.”

Neema alianza kazi hiyo kwa bidii na akaendelea kuishi kwa unyenyekevu, akisaidia wengine kama alivyofanya tangu awali sasa akiwa na uwezo zaidi.

emakulatemsafiri@gmal.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments