BIDII NA NIDHAMU HULETA MAFANIKIO

Emakulata Msafiri

Suzana aliishi mjini pamoja na familia yake. Ndoto yake kubwa ilikuwa kufaulu masomo ili siku moja awe mwalimu na kufundisha watoto wengine.

Lakini watoto wenzake walimcheka. Wakamwambia “Wewe huna kitu utawezaje kuwa mwalimu? Bora ucheze kuliko kusoma sana.”Maneno hayo yalimuumiza lakini Suzana hakukata tamaa. Aliamua moyoni.

“Sitakubali mtu yeyote aniue ndoto. Nitasoma kwa bidii kwa sababu ndoto yangu ni ya maana.”

Kila siku alisoma vitabu vyake kabla ya kwenda kucheza. Usiku alikaa karibu na taa ndogo akisoma kwa moyo wote. Walimu wake waliona bidii yake wakampatia vitabu vya ziada na kumtia moyo.

Wakati wa mitihani ulipofika Suzana alifanya vizuri sana. Alipata alama za juu kuliko wengi. Wale waliomcheka walishangaa sana na kusema,

“Tulidhani huwezi kumbe ndoto zako ni kubwa kuliko maneno yetu.”

Suzana akatabasamu na kusema, “Msikubali mtu yeyote awakatishe ndoto zenu. Mkisoma kwa bidii na kuamini, mtafanikiwa.”

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments