AMANI YA KWELI HUPATIKANA KWA UPENDO

Emakulata Msafiri

Kulikua na Familia hii iliyoishi katika nyumba ndogo ya udongo lakini ilikuwa safi sana yenye maua ya kupendeza pembeni mwa mlango na kiti cha kamba cha kupumzikia. Ingawa hawakuwa na mali nyingi walikuwa na kitu kimoja cha thamani amani.

Kila asubuhi wlikuwa wakiamka kwa sala na shukrani. Watoto walisaidia kazi ndogondogo kama kufagia, kuchota maji na kulisha kuku. Walicheka pamoja, walila pamoja na walizungumzia matatizo yao kwa utulivu.

Siku moja jirani yao aitwaye Bwana Shaka aliyekuwa na nyumba kubwa ya kisasa aliwaambia:

“Kwa nini mnacheka sana ilhali nyumba yenu ni ndogo? Hamna runinga kubwa wala gari!”

Mzee Baraka alitabasamu akasema “Bwana Shaka siisi tuna kitu kikubwa zaidi ya runinga tuna amani, upendo na mshikamano. Hivyo maisha yetu ni mazuri.”

Bwana Shaka alishtuka. Alikuwa na mali nyingi lakini nyumbani kwake kila mtu alikuwa na hasira, waligombana kila siku na hakuna aliyekuwa na furaha.

Baada ya siku kadhaa Bwana Shaka alianza kujifunza kutoka kwa familia ya Mzee Baraka. Alianza kuzungumza kwa upole na familia yake, kusali nao, kula nao pamoja na kufurahia muda pamoja. Polepole hata nyumba yao ilianza kuwa na amani.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments