AKILI NI SILAHA KULIKO NGUVU


Emakulata Msafiri

Kulikuwa na nyati mmoja aliyekuwa akiishi katika pori moja kubwa lenye nyasi ndefu na miti mirefu. Nyati huyu alikuwa si mkubwa sana kama wenzake lakini alikuwa na kitu kimoja cha kipekee alikuwa mjanja sana.

Nyati huyu aliitwa Mjeuri. Wanyama wengine walimcheka mara nyingi kwa kuwa hakuwa na nguvu nyingi lakini yeye hakuwajali. Alijua kuwa akili ni silaha kali zaidi kuliko nguvu.

Siku Moja Simba mmoja mwenye njaa kali alitokea katika pori lile. Alikuwa ametembea siku tatu bila chakula. Alipomuona Mjeuri akichunga majani kando ya mto alinyemelea kimya kimya ili amshambulie.

Lakini Mjeuri alimsikia Simba kabla hajamfikia.Badala ya kukimbia Mjeuri alijifanya haoni chochote. Simba aliposogea karibu Mjeuri alianza kuzungumza peke yake kwa sauti ya juu:

"Nafikiri simba huyu mkubwa niliyekamata jana alinikosea. Alifikiri atanila mimi kumbe nimemchinja na ngozi yake ndiyo hii navaayo leo! Hawa simba wa siku hizi hawana adabu."

Simba aliposikia hayo alisimama kwa mshangao. Akajiuliza:

“Kama nyati huyu mdogo aliweza kumchinja simba mwingine basi si wa kawaida. Labda ni mchawi au shujaa mkubwa!”

Simba aligeuka na kukimbia kwa kasi kupita upepo!



Tangu Siku hiyo Wanyama wote walimsifu Mjeuri kwa ujanja wake. Aliendelea kuishi salama porini bila kuumizwa kwa sababu kila mnyama alifikiri ana nguvu za ajabu kumbe ni akili tu!

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments