Emakulata Msafiri
Palikuwa na mvulana mdogo aitwaye Yohana. Alikuwa mtiifu lakini siku moja alijaribiwa sana. Katika kijiji chao Malkia alikuwa na kuku wa kipekee aliyekuwa akitaga mayai ya dhahabu. Malkia alitangaza:
“Atakayepata yai la dhahabu na kuileta kwangu atapewa zawadi kubwa!”
Siku moja asubuhi, Yohana alipokuwa akitembea karibu na bustani ya kifalme aliona kitu kikimetameta kwenye nyasi. Alipokichukua alishangaa kilikuwa yai la dhahabu! Lakini hakuwa na hakika kama ni lake au la kuku wa malkia.
Watu wengine walimwambia:
“Usilipeleke! Liweke nyumbani ulichome utapata utajiri.”
Lakini moyo wa Yohana ulimuuma. Aliamua kulipeleka kwa malkia.
Malkia alifurahi sana. “Yai hili lilipotea kwa siku mbili! Umeonyesha uaminifu mkubwa.”
Badala ya zawadi ya kawaida malkia alimpa Yohana kazi maalum kuwa msimamizi wa bustani ya kifalme. Alipata elimu, chakula na heshima kubwa kwa sababu ya kusema ukweli.
emakulatemsafiri@ gmail.com
0653903872
Post a Comment