Emakulata Msafiri
Kuliku na mtoto mmoja mrembo na mpole aitwaye Amina. Amina alikuwa maarufu kwa kuwa na adabu nzuri sana. Alisalimia watu wote aliwasaidia wazee kubeba mizigo na hakuwahi kujibu watu kwa hasira.
Kila mtu kijijini alimpenda Amina. Lakini wengine walimcheka wakisema,
“Kwa nini uwe na adabu sana? Haina faida!”
Siku mojav kijiji kilikumbwa na tatizo la mvua ilikataa kunyesha kwa miezi mingi. Wakulima walihangaika, wanyama walikufa kwa kiu na watu walipoteza matumaini.
Mzee mmoja mwenye busara aliwaita watoto wa kijiji na kusema:
“Yupo mtoto mmoja tu mwenye moyo safi na adabu atakayechagua jiwe la mvua kutoka msituni. Jiwe hilo likiletwa hapa mvua itanyesha tena.”
Watoto wengi walikwenda msituni kutafuta jiwe hilo lakini kila walipolishika lilikuwa linapotea. Amina naye alienda kwa utulivu akasalimia msitu kwa heshima na alipoliona jiwe aliliinua kwa upole na kusema:
“Ewe jiwe la mvua, rudi nasi kwa upendo!”
Kwa mshangao jiwe hilo liliangaza mwanga wa bluu na mvua ilianza kunyesha mara moja! Watu walishangilia na kusema “Adabu ya Amina imetuokoa!”
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment