Emakualata Msafiri
Filamu za katuni hupendwa sana na watoto kwa sababu huwa na vichekesho, rangi nzuri na visa vya kusisimua. Katuni nzuri zinaweza kuwalea watoto kwa njia bora kwa kuwafundisha tabia kama kusema kweli, kusaidiana kutii wazazi na kujifunza lugha mpya. Mfano ni katuni kama Dora the Explorer au Paw Patrol ambazo hufundisha ushirikiano ujasiri na upendo.
Zaidi ya hayo katuni huchangamsha akili za watoto na kuwafanya wafurahie kujifunza kupitia michezo na nyimbo. Watoto wanaotazama katuni nzuri hukua wakiwa wacheshi wachangamfu na wapenda amani.
Hata hivyo si katuni zote ni nzuri. Baadhi zina vurugu kelele nyingi na maneno mabaya. Watoto wanaweza kuiga tabia hizo bila kuelewa madhara yake. Wengine huanza kuwa wakorofi, wasiosikiliza wazazi au walimu, na hata kupenda kupigana. Pia kuangalia katuni kupita kiasi huwafanya watoto kusahau kusoma, kufanya kazi za nyumbani au kucheza nje.
Kwa hiyo ni vizuri wazazi kuwachunga watoto wao na kuhakikisha wanaangalia katuni zenye mafunzo mazuri. Pia waweke muda maalum wa kuangalia ili watoto waweze kujifunza, kusaidia nyumbani na kupata muda wa kupumzika.
Kwa kumalizia movie za katuni zinaweza kulea watoto kwa njia nzuri au mbaya. Inategemea ni katuni gani na namna mtoto anavyolelewa anapotazama.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment