Emakulata Msafiri
Kuna siku moja kobe mdogo alikuwa akitembea kando ya mto. Wanyama wengi walimcheka kwa sababu alikuwa akitembea polepole sana.
"Angalia huyu kobe! Polepole kama jiwe!" walimsema ndege na tumbili waliokuwa karibu.
Kobe hakujali. Aliendelea na safari yake kwa utulivu na akafika karibu na maji. Gafla, aliona kijana wa tumbili akiteleza na kuanguka majini.
Tumbili alianza kuita msaada lakini wanyama wengine waliogopa kuingia majini. Kobe bila kuogopa akaogelea taratibu na kumsaidia tumbili kutoka majini.
Wanyama wote walishangaa. Wale waliomcheka awali waliona jinsi kobe alivyokuwa jasiri na mwenye moyo wa huruma.
Baada ya hapo, wote walimshukuru kobe na kuacha kumdharau.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment