USIDANGANYIKE NA MWONEKANO


Emakulata Msafiri

Kulikua njiwa mmoja mzuri sana aliyekuwa akiishi kwenye mti mkubwa karibu na kijiji. Kila siku njiwa huyo aliruka angani kutafuta chakula kisha kurejea kwenye mti wake kupumzika.

Siku moja alipokuwa akiruka akitafuta chakula aliona nafaka nyingi sana zimezagaa chini ya mti mmoja. Alishangaa kuona chakula kingi namna ile lakini njaa ilimfanya ashuke haraka bila kufikiri sana.

Aliposhuka chini na kuanza kula mara mtego uliokuwa umefichwa kwenye nyasi ulimnasa miguu yake! Njiwa alijaribu kujitoa lakini alishindwa. Alilia kwa huzuni “Ewe Mungu nisaidie!”

Bahati nzuri kulikuwa na kunguru aliyekuwa amemwona kutoka juu ya mti. Kunguru huyo aliruka haraka na kumtoboa kamba za mtego kwa domo lake. Njiwa akaweza kuachika na kuruka juu kwa furaha.

Alimshukuru kunguru na kusema “Nimejifunza kuwa si kila kitu kinachong’aa ni dhahabu. Nitakuwa mwangalifu siku nyingine.”



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments