Emakulata Msafiri
Kulikuwa na kijiji kidogo kilichozungukwa na milima na misitu. Kijijini humo aliishi mama mmoja mjane aitwaye Mama Ashura pamoja na mtoto wake pekee Ashura. Mama Ashura alimpenda sana Ashura lakini alikuwa na tabia ya kumkosoa na kumlaumu kwa kila kitu.
Siku mojaMama Ashura alitoka sokoni na kununua chungu cha asali safi. Alipofika nyumbani akakiweka juu ya meza na kumwambia Ashura:
"Usiguze hii asali maana hujui kuishika vizuri utaimwaga!"
Ashura alijaribu kujizuia lakini alihisi harufu tamu ya asali ikimvutia. Baada ya muda aliamua kuonja kidogo tu. Kwa bahati mbaya chungu kikaanguka sakafuni. Mama Ashura aliporudi alimkuta Ashura akilia na sakafu ikiwa na asali kila mahali.
Mama Ashura alikasirika sana, akamfokea Ashura:
"Umeshindwa hata kitu kidogo! Wewe ni mtoto mzembe, sitaki kukuona!"
Ashura akakimbia nje kwa hofu. Alikimbia mpaka msituni akakaa chini ya mti akilia. Mzee mmoja aliyekuwa akipita akamkuta na kumuuliza:
"Mbona unalia binti yangu?"
Ashura akamueleza yote. Mzee akamwambia kwa upole:
"Usihuzunike. Wazazi wakati mwingine wanakosea kwa hasira zao. Anapaswa kukuonyesha upendo na kukusamehe si kukufukuza."
Mzee alimrudisha Ashura nyumbani. Mama Ashura alipomuona binti yake amerudi alilia kwa uchungu. Akatambua kosa lake na kumkumbatia Ashura:
"Samahani mwanangu. Nilikosea. Nilipaswa kukufundisha si kukukemea kwa hasira."
Kuanzia siku ilenMama Ashura alijifunza kuwa mzazi bora na alimfundisha kwa upendo alijua kuwa watoto hukosea kama wanavyokosea watu wazima.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment