TAMAA MBAYA

 


Emakulata Msafiri

 Mbwa na Paka walikuwa marafiki wakubwa. Waliishi pamoja kwa amani na walishirikiana kila kitu. Walikula pamoja, walilala pamoja na hata walicheza pamoja.

Siku moja walikuwa na chakula kidogo tu kilichobaki kipande kimoja cha nyama. Wote walikitamani lakini walikubaliana kwamba lazima wagawane haki sawa.

Mbwa akasema, “Tunaweza kumwita Kima atuhukumu, yeye ni mwerevu na atagawa sawa.”

Walipompelekea Kima nyama, Kima akasema “Ngoja nitumie mizani yangu.”

Akaweka kipande kimoja upande wa kushoto na kingine upande wa kulia lakini akasema, “Ah! Kipande hiki ni kizito zaidi,” akakila kipande kidogo ili vipande viwe sawa.

Kisha mizani ikawa upande wa pili, akasema tena, “Ah! Sasa hiki ni kikubwa kuliko kingine!” Akakila tena upande mwingine.

Alirudia hivyo hadi nyama yote ikaisha!

Mbwa na Paka walitazamana kwa mshangao. “Kima! Umekula nyama yote!”

Kima akasema, “Msijali. Nimehakikisha haki imetendeka.”

Tangu siku hiyo, Mbwa na Paka waliamua kutomwamini tena Kima na pia walikosa kuwa marafiki wa karibu kama zamani.


emakulatamsafiri@gmail.com

0653903872

-


0/Post a Comment/Comments