Emakulata Peter
Kulikua na kijiji kimoja aliishi babu mmoja mzee mwenye hekima ajulikanaye kama Babu Mwasapile. Babu huyu alikuwa na kikombe kimoja cha ajabu. kikombe cha miujiza kilichotibu magonjwa yote duniani. Alipata kikombe hicho baada ya kuota ndoto ambapo alioneshwa mmea wa dawa unaoitwa Mugariga.
Babu alianza kuwakaribisha watu kutoka kila kona. Watu waliokuwa wagonjwa walikuja kwa foleni ndefu. Kila mmoja alipewa kikombe kimoja cha dawa ya mimea. Babu aliwaambia:
“Kikombe hiki kitakutibu lakini ni kwa wale walio na mioyo safi wasio na chuki na wanaoamini.”
Watoto, wazee na hata wanyama walianza kupona! Lakini Babu hakutaka pesa wala zawadi alisema:
“Msaada wa kweli ni kuishi kwa upendo na kusaidiana.”
Kijana mmoja mwerevu aitwaye Zawadi alijifunza kutoka kwa Babu kwamba dawa ya kweli si kikombe tu bali ni tabia njema, usafi na matumaini. Baada ya muda babu alitoweka kimiujiza msituni na kikombe chake kilihifadhiwa kwenye pango lenye mwanga wa dhahabu. Ilisemekana kuwa kikombe hicho kitaonekana tena pale ambapo watoto wataishi kwa upendo, ukweli na huruma.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment