Emakulata Msafiri
Mtaa mmoja wa mjini unaoitwa Mtaa wa Jua Kali. Mtaa huo ulikuwa na taa chache na baadhi ya nyumba zilikuwa hazikamiliki ujenzi. Watoto wengi walipenda kucheza hadi jioni lakini walionywa kurudi mapema kabla ya giza kuingia.
Siku moja watoto wanne Amina, Juma ,Rachel na Tobi waliamua kucheza mpira hadi usiku licha ya onyo la wazazi wao. Wakiwa wanarudi nyumbani walipita karibu na jengo la zamani lililoachwa bila kukamilika. Jengo hilo lilihusishwa na uvumi kwamba lilikuwa na "sauti ya usiku" ambayo humuita mtu mmoja mmoja na kumfanya apotee.
Wakiwa wanapita ghafla wakasikia sauti ya kike ikisema kwa upole:
"Tobi... Tobi... njoo hapa..."
Tobi alisimama ghafla macho yake yakabadilika rangi na kuwa meupe kana kwamba haoni wenzake. Akaanza kutembea kuelekea kwenye jengo lile. Amina na Juma walimpigia kelele lakini hakuwa anasikia. Walimfuata kwa hofu.
Ndani ya jengo kulikuwa na giza baridi kali na harufu ya unyevu. Walipoingia kumfuata Tobi, mlango wa jengo ukajifunga ghafla kwa kishindo! Walipiga kelele lakini hakuna mtu aliyesikia. Mara wakasikia vicheko vya ajabu vikisikika ukutani kama sauti za watoto waliopotea
Rachel alitoa rozari aliyokuwa amevalia shingoni akaanza kusali kwa sauti ya hofu. Ghafla taa moja iliwaka juu yao na Tobi akazinduka kana kwamba ametoka usingizini. Mlango ukafunguka taratibu nao wakakimbia kwa nguvu kurudi nyumbani bila hata kugeuka nyuma.
Tangu siku hiyo watoto wote walikubali kuwa jiji lina sehemu za kutisha na si kila mahali pa kuchezea hadi usiku. Wakaapa kutowahi kuchelewa tena barabarani.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment