Emakulata Msafiri
Je, unamfahamu panya mdogo aitwaye Pendo. Alikuwa na ndoto kubwa sana alitaka kuwa mpishi maarufu katika msitu mzima. Lakini kila alipojaribu kupika wanyama wengine walicheka.
"Mpishi? Wewe ni panya tu!" walimsema fisi na nyani.
"Unapika chakula cha panya hakuna anayekitaka!" aliongeza tumbili huku akicheka.
Lakini Pendo hakukata tamaa. Kila siku alijifunza kupika kwa kutumia matunda mboga na viungo vya porini. Alijaribu na kushindwa mara nyingi lakini hakukata tamaa.
Siku moja kulikuwa na sherehe kubwa ya msitu. Simba mfalme wa msitu, alitangaza kuwa kuna nafasi ya mpishi mmoja tu kupika chakula cha wageni.
Wanyama wengi walijaribu lakini chakula cha Pendo kilipendeza sana! Kilikuwa kitamu chenye harufu nzuri na kilitengenezwa kwa upendo.
Simba alisimama na kusema kwa sauti:
“Mpishi bora ni... Pendo panya mdogo mwenye ndoto kubwa!”
Wanyama wote walishangaa na kupiga makofi. Tangu siku hiyo Pendo akawa mpishi maarufu msituni na kila mnyama alijifunza kuwa ndoto yoyote inaweza kutimia hata kama wewe ni mdogo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment