Emakulata Msafiri
Kulikuwa na mtoto mmoja anayeitwa Neema. Neema alipenda sana kucheza hadi giza linaingia, hata kama wazazi wake walimkataza.
Siku moja baada ya jua kuzama Neema aliamua kutoka nje kuokota maua aliyoyaona mchana. Alijua kabisa kuwa haipaswi kutoka usiku lakini alijisemea, "Nitakimbia haraka hakuna cha kunishika."
Alipokuwa akitembea alisikia kitu kinachosogea nyuma yake. Aliposimama kitu hicho kilisimama. Alipoanza kutembea nacho kilitembea. Neema akageuka kwa kasi akaona kivuli kirefu chenye macho mekundu kikimfuata.
Neema akaanza kukimbia miguu yake ikitetemeka. Kivuli kile kilikuwa kinapiga hatua ndefu, kikimkaribia. Neema akapiga kelele lakini hakuna aliyemsikia. Ghafla kivuli kikamgusa bega… na mara akahisi baridi kali mno ikimzunguka.
Baada ya hapo, Neema hakutoka tena usiku. Aliwaambia watoto wengine, "Msithubutu kutoka usiku kuna kitu kinaishi gizani kinapenda kuwakamata watoto wasiotii."
Na tangu siku hiyo watoto wote walikaa ndani kabla ya giza kuingia.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment