MTOTO USIMNYIME MAPIGO

Emakulata Msafiri

Wazazi wengi wamewahi kusikia msemo huu: "Mtoto usimnyime mapigo." Lakini unamaanisha nini hasa? Je, ni vizuri kumpiga mtoto kweli?

Msemo huu unatokana na imani za zamani kuwa mtoto anayeadhibiwa kwa viboko kidogo anakua mnyenyekevu, mwenye nidhamu na anayeheshimu watu wazima. Wazazi walikuwa wanaamini kuwa mtoto asipoonywa kwa fimbo atakuwa mkaidi na hafai katika jamii.

Hata hivyo leo tunajua kuwa kuna njia nyingine bora za kumlea mtoto bila kutumia mapigo. Wataalamu wa malezi wanasema adhabu ya kimwili inaweza kumfanya mtoto kuwa na woga, kutojiamini, na hata kuwa mkorofi zaidi. Badala ya fimbo, wazazi wanaweza kutumia:

Kumueleza mtoto kosa lake kwa upole,Kumpa muda wa kutulia (time out), Kumkatalia vitu anavyopenda kama adhabu ya kujifunza na Kumfundisha kwa mfano vote hivi vinamsaidi kua mtoto mwenye adabu na hekima.

Poa mtoto anapopata upendo na maelekezo mazuri anakua mtu mzuri anajiamini na ana hofu ndogo. Mapenzi na maelezo yana nguvu kuliko viboko!

Kwa hiyo, ingawa msemo unasema "Mtoto usimnyime mapigo", tusisahau kuwa lengo si kumuumiza, bali kumlea kwa hekima

Kila mzazi anatakiwa kumfundisha mtoto nidhamu lakini si lazima kutumia fimbo. Upendo, uvumilivu, na mazungumzo ndiyo silaha bora za malezi bora.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments