MTOTO MWEREVU ALIYETIMIZA NDOTO ZAKE

Emakulata msafiri

Amina alikuwa msichana mdogo aliyeishi na mama yake katika mtaa wa Buguruni jijini Dar es Salaam. Waliishi katika chumba kimoja na maisha yao hayakuwa rahisi. Mama yake alikuwa muuza maandazi na Amina alisaidia kila asubuhi kabla ya kwenda shule.

Ingawa maisha yalikuwa magumu Amina hakuwahi kulalamika. Alikuwa mwerevu darasani na kila siku alisoma kwa bidii, hata kwa mwanga mdogo wa kibatari usiku.

Marafiki zake wengine walimcheka.

“Wewe unasoma sana lakini huna hata daftari jipya!”

Amina alitabasamu tu. “Elimu ni taa yangu. Siku moja nitakuwa daktari.”

Mwalimu wake alimpenda sana kwa juhudi zake. Siku moja, shule yao ilitangaza mashindano ya insha. Amina aliandika kuhusu ndoto yake ya kuwasaidia watoto wa mitaani. Insha yake ilichaguliwa kuwa bora katika wilaya nzima!

Baada ya hapo alipata ufadhili wa kusoma shule ya sekondari nzuri jijini. Amina aliendelea kuwa mvumilivu na mwenye bidii. Miaka michache baadaye ndoto yake ilitimia alikua daktari na alifungua zahanati katika mtaa aliokulia.

Watoto waliomcheka zamani walimwangalia kwa heshima. Alikuwa mfano wa kuigwa.


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments