MTOTO MPOLE ANAYEPENDWA NA WATU

Emakulata Msafiri

Mtoto mmoja aitwaye Rashid. Rashid alikuwa na umri wa miaka saba tu, lakini tabia yake ilikuwa ya kipekee. Alijulikana kwa upole wake, unyenyekevu na kusaidia watu bila kutarajia malipo yoyote.

Kila siku Rashid alipomaliza kazi zake za shule, alikuwa na tabia ya kuwasaidia wazazi wake kazi za nyumbani. Aliwapikia wanyama, kufagia uwanja na wakati mwingine hata kuwasaidia majirani waliokuwa na uhitaji. Hakuwahi kupenda ugomvi wala kutukana wenzake. Hata pale alipochezewa vibaya Rashid alichagua kusamehe badala ya kulipiza.

Siku moja shule yao ilitangaza mashindano ya kuchagua mtoto mwenye tabia njema zaidi. Walimu waliamua kuwahoji wanafunzi na walinzi wa shule kuhusu tabia za watoto wote. Jina la Rashid lilitajwa na kila mtu aliyefikiwa.

Mwalimu mkuu alipopewa majina bila kusita alimtangaza Rashid kuwa mtoto bora wa mfano. Alipigiwa makofi mengi na wenzake na alipandishwa jukwaani akapewa zawadi ya daftari, kalamu na cheti cha heshima. Rashid alipokuwa akizungumza mbele ya hadhira alisema kwa unyenyekevu, “Nashukuru kwa heshima hii. Nimefundishwa kuwa mpole, mtii na mwenye kusaidia wengine. Kila mtu anaweza kuwa bora kwa kuwa na tabia nzuri.”

Tangu siku hiyo watoto wengi katika kijiji hicho walianza kumuiga Rashid. Waligundua kuwa tabia nzuri huleta upendo, heshima na nafasi nzuri maishani. Rashid aliendelea kuwa mfano mzuri hata alipokuwa mkubwa na baadaye alikuja kuwa kiongozi mzuri wa kijiji chao.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments