MPIRA WA MIGUU KWA WATOTO

 

Emakulata Msafiri

Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa sana duniani na hasa na watoto. Kila siku baada ya masomo watoto wengi hukimbilia viwanjani kucheza mpira na marafiki zao.

Mpira wa miguu unasaidia watoto kupata afya bora. Watoto wanapocheza mpira miili yao inapata mazoezi, hii inasaidia kuimarisha misuli na mifupa na pia huzuia magonjwa kama unene kupita kiasi.

Lakini pia mpira wa miguu huwafundisha watoto nidhamu na uvumilivu.Wanajifunza kwamba kushinda si jambo rahisi hivyo wanajifunza kuvumilia wanaposhindwa na kujaribu tena bila kukata tamaa

Mpira wa miguu unawafundisha watoto umuhimu wa ushirikiano. Katika mpira mchezaji hawezi kucheza peke yake na kushinda. Watoto hujifunza kusaidiana kupiga pasi na kupanga mikakati ya pamoja. Mchezo huu huwafanya kuwa na moyo wa upendo na umoja.

Vilevile mpira wa miguu huleta furaha kubwa. Wakati watoto wanapocheza wanacheka na kufurahia muda wao. Unawasaidia kupunguza mawazo mabaya na msongo wa mawazo.

Kwa ujumla mpira wa miguu ni mchezo muhimu sana kwa watoto. Unawasaidia kuwa na afya, kujenga nidhamu, kuimarisha urafiki, na kupata furaha. Watoto wote wanashauriwa kucheza mpira au kushiriki michezo mingine ili wawe na maisha bora na yenye furaha.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments