Emakulata Msafiri
Mjini Dar es Salaam aliishi mama mmoja na mtoto wake Kai. Kai alikuwa mvulana mzuri lakini alikuwa na tabia moja mbaya ya ubishi.
Mama yake alikuwa anafanya kazi ya kuuza vitumbua sokoni na kila siku alikuwa akimwambia Kai “Kai usitoke nje ya geti ukiwa peke yako. Mji ni mkubwa na magari ni mengi unaweza kupata ajali.”
Lakini Kai hakutaka kusikia. Aliona kama mama yake anamnyima uhuru. Alipenda sana kucheza mpira na marafiki zake barabarani.
Siku mojab mama yake alipokuwa kazini Kai aliona marafiki zake wakicheza mpira upande wa pili wa barabara. Bila kufikiria mara mbili alikimbia kutoka ndani akafungua geti na kukimbia barabarani.
Ghafla gari moja lilikuwa linakuja kwa kasi. Dereva alijaribu kumkwepa lakini Kai aliogopa na kusimama katikati ya barabara. Kwa bahati nzuri boda boda aliyekuwa karibu alimvuta haraka na kumuepusha na ajali.
Watu waliokusanyika walimpeleka Kai nyumbani. Mama yake aliporudi, alimkuta Kai anahema kwa woga na machozi yakimtoka.Kai alitambua kosa lake na akaomba msamaha. Aliahidi kumsikiliza mama yake kila siku na kutotoka nje bila ruhusa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment