MCHEZO WA KARATA KWA WATOTO

Emakulata Msafiri

Mchezo wa karata ni moja ya michezo ninayoipenda sana. Ni mchezo rahisi unaochezwa na watoto wawili au zaidi. Mchezo huu hufurahisha sana na pia husaidia kuongeza kumbukumbu na umakini.

Katika mchezo wa karata kuna karata zenye picha mbalimbali. Kila picha huwa ina jozi yake. Karata hizi huchanganywa kisha kuwekwa chini zikiwa zimefunikwa ili picha zisionekane. Kila mtoto huchukua zamu ya kufungua karata mbili. Kama karata hizo zinafanana mtoto huyo huzichukua na kupata alama. Akikosea hufunika tena na kumpa mwingine nafasi ya kujaribu.

Mchezo huu unahitaji akili na kumbukumbu nzuri. Unatufundisha kuwa makini na kukumbuka tulipoziona picha zilizopita. Pia hutufundisha kuwa wavumilivu tunapocheza kwa zamu.

Ninapocheza mchezo huu na marafiki zangu tunafurahi sana. Wakati mwingine tunacheka hadi machozi yanatutoka. Huu ni mchezo unaofaa sana kwa watoto wa rika langu. Nimependa mchezo wa karata kwa sababu unanifurahisha na kunisaidia kujifunza vitu vingi muhimu.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments