Emakulata Msafiri
Aliishi ndege mmoja mkubwa sana aitwaye Mbuni. Mbuni alikuwa na mwili mkubwa lakini hakupenda kuruka kama ndege wengine. Alijiona bora kuliko wote kwa sababu alikuwa na kasi sana alipokuwa akikimbia ardhini.
Siku moja ndege wengine walikutana na kujadili safari ya kwenda pori la mbali lililojaa chakula kingi. Waliamua kuruka angani kwenda huko. Walipomwalika Mbuni, Mbuni alisema kwa majivuno “Mimi sihitaji kuruka nitafika kwa miguu yangu ya haraka!”
Safari ilianza ndege wote wakapaa juu wakapita juu ya milima na mito. Mbuni akaanza safari yake kwa kukimbia chini. Mwanzoni alikuwa na kasi sana lakini baadaye alichoka. Alikutana na simba njiani akalazimika kujificha. Mvua kubwa ikanyesha barabara zikawa na tope.
Wakati wenzake walifika salama porini na kufurahia matunda Mbuni alikuwa bado njiani, amechoka amepotea na hana chakula. Alijuta kwa nini hakukubali msaada wa wenzake.
Tangu siku hiyo, Mbuni alijifunza kuwa kiburi hakisaidii na ni vizuri kushirikiana na wengine na kukubali ushauri.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872



Post a Comment