KUKU NA KOFIA YA RANGI

Emakulata Msafiri

Siku moja kulikuwa na kuku mmoja anayeitwa Kido. Kido alikuwa anapenda sana kuvaa kofia. Lakini si kofia za kawaida kofia zake zilikuwa za rangi nyingi nazo ni nyekundu, kijani, njano na hata pinki!

Siku moja Kido aliamua kwenda sokoni kuvaa kofia yake mpya ya bluu. Alipofika sokoni wanyama wote walimshangaa:

Mbwa: "Wow! Kido, hiyo kofia yako ni ya kisasa kweli!"

Paka: "Naweza kuazima kesho? Nina harusi ya paka!"

Mbuzi: "Hee! Nisingeweza kukutambua bila hiyo kofia!"

Kido alijivunia sana. Alitembea sokoni akipiga hatua za madaha huku akipunga mkia wake. Lakini ghafla upepo mkali ukavuma!

Kofia yake ilirushwa juu juu ikapaa juu ya mti wa embe! Kido akapiga kelele:

"Oooi! Kofia yangu! Msaada!"

Kisha ndege mdogo anayeitwa Tido akateremka kutoka mti akamshushia kofia.

Kido akasema: "Asante sana Tido! Bila wewe ningekuwa kichwa wazi leo!"

Wanyama wote wakaanza kucheka kwa furaha.

Kuanzia siku hiyo, Kido aliamua kushika kofia yake vizuri kila mara anapotoka.

Na kuanzia siku hiyo Kido akawa anajulikana kama "Kuku wa Kofia" na alikua maarufu sokoni.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments