KUJARIBU NI HATUA YA KWANZA YA KUFANIKIWA



Emakulata Msafiri

Mwanakwetu Kids

Siku mojabkulikuwa na sherehe kubwa kijijini . Watoto wengi walialikwa na kulikuwa na michezo mingi ya kufurahisha. Mwalimu Abdul alisema :

"Leo tutafanya mashindano ya kukimbia na magunia! Mshindi atapata zawadi ya pipi tamu na mpira mpya!"

Watoto wote walishangilia, "Ndiyo! Ndiyo!"

Happy alikuwa na wasiwasi kidogo kwa sababu hakuwahi kukimbia na gunia hapo awali. Lakini rafiki yake Juma alimshika mkono na kusema

"Usiogope Happy! Tujaribu pamoja!"


Watoto walivaa magunia yao, wakaingia ndani, na kusubiri ishara ya kuanza.

Mwalimu alipiga kengele: "Start!"

Wote walianza kuruka wengine wakaangukab wengine wakaendelea kucheka. Happy alianza kwa taratibu lakini akajitahidi kuruka kwa nguvu na kwa uangalifu.

Ghafla alijikuta yupo mbele! Juma naye aliruka kwa kasi akimfuata. HatimayebHappy akafika mstari wa mwisho wa kushinda. Wote walimshangilia:

"Happy! Happy! Hongera!"

Mwalimu Abdul alimpa pipi tamu na mpira mpya. Happy alifurahi sana na alisema,

"Sasa nimejua kuwa nikijaribu ninaweza!"

Wote walijifunza kwamba mchezo si kushinda tu bali kufurahia na kusaidiana.




emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments