KIUMBE WA USIKU

 


Emakulata Msafiri

Mariam, Shabani na Asha walikuwa marafiki wakubwa. Kila siku walipenda kucheza mpira na kukimbizana hadi jua linapozama.

Siku moja wliendelea kucheza bila kujali muda. Wakati jua lilipozama, waliona giza linaingia polepole. Walipoanza kurudi nyumbani, ghafla walisikia sauti ya ajabu kutoka msituni:

 "Woooo... Woooo..."

Walisimama kwa hofu. Mara wakaona macho mekundu yakimetameta kwenye vichaka. Kisha kivuli kirefu kikaanza kusogea karibu nao.

Kwa woga walipiga kelele na kukimbia kwa kasi sana. Walifika nyumbani wakiwa wanatetemeka na kupumua kwa shida.

Mama alimwambia Mariam:

 “Niliwaonya msichelewe kurudi! Usiku kuna viumbe vya ajabu vinavyotembea msituni.”

Tokea siku hiyo, watoto hao walirudi nyumbani mapema kila siku na hawakuthubutu kuchelewa tena.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments