JIVUNIE JINSI ULIVYO

Emakuata Msafiri

Kulikuwa na kinyonga mdogo aitwaye Kito,aliyeishi kwenye mti mkubwa kando ya mto. Kito alikuwa tofauti na wanyama wengine kwa sababu alikuwa akibadilika rangi kulingana na mahali alipo. Lakini Kito hakuipenda hali hiyo. Alitamani awe na rangi moja tu kama simba au twiga.

“Sipendi kubadilika badilika,” Kito alilalamika. “Nataka kuwa wa rangi ya dhahabu kila siku!”

Siku moja alienda kwa bundi mzee aliyejulikana kwa busara zake. “Bundi naomba unisaidie. Nataka kuwa wa rangi moja tu!”

Bundi alimwangalia kwa upole. “Lakini Kito kubadilika kwako ni zawadi si laana. Unajua kwa nini?”

Kito alitikisa kichwa.

“Kwa sababu unaweza kujificha na kujilinda. Unaweza kubeba rangi yoyote unayopenda. Na muhimu zaidi unaweza kuishi kwa namna ambayo wengine hawawezi. Hilo ni jambo la kipekee!”

Kito alifikiria kwa muda halafu akaanza tabasamu. Alielewa kuwa kila mmoja ana zawadi yake ya kipekee. Tangu siku hiyo kito alijifunza kujipenda alivyo na akawasaidia viumbe wengine kuelewa thamani ya kile walicho nacho.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments