Emakulata Msafiri
Kulikua na mfalme aliyejulikana kwa jina la Suji na pia alikua na watoto wawili wa kike majina yao ni Bigda na Bidu. Mfalme alikua anatabia moja mbaya sana kwasabab aliwatumikisha wanakijiji kwa mabavu na aliamini hawana chochote cha kufanya kwasababu alikua mtawala
Siku moja aliandaa sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa wanae na aliwaambia migambo wapige mbiu ili kila mwanakijiji ashiriki sherehe hiyo.
"Lamgambo lamgambo likilia ujue kuna jambo Mfalme wetu anawaalika watu wote mshiriki katika sherehe ya watoto wake na asipange mtu kukosa".
Muda wa sherehe ulipofika wanakijiji hakuenda waliendelea na majukumu yao ya kila siku kwasababu mfalme alikua na roho mbaya na haukuna mtu aliyetaka kumkaibia.
Watoto walianza kumuliza baba yao; Baba kwhiyo sherehe yetu haina wanakijiji na mbona chakula kingi kimepikwa na watumwa inamaa tutakimwaga baada ya sherhe kuisha? Baba aliona haya kujibu alitoka nje na kuchukua wafuasi wake na kwenda kutangazaa tena.
"Wanakijiji wote naomba mshiriki katika sherehe ya watoto wangu kwasababu watakua wapweke na tumepika chakula kingi sana"
Wanakijiji walivyosikia hivyo waliamua kwenda kwenye sherehe hiyo na walipofika mfalme alifurahi sana na kuwaomba jambo
"Nachukua nafasi hii kuwaomba wanakijiji tuishi kwa amani na upendo na mimi tabia yangu ninarekeisha kuanzia leo kwasababu wanangu wamenifunza kitu kikubwa sana sana nawapenda wote wananchi wangu
Wanakijiji walifurahi sana na kumpigia makofi mfalme wao. Tangu siku hiyo waliishi kwa amani na upedo na kijiji hicho kilikua mfano wa kuigwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment