HISTORIA YANGU

Emakulata Msafiri

Mimi nilifundishwa kucheza bao na babu yangu. Alinieleza kuwa bao si mchezo wa kukimbilia ushindi bali ni wa kufikiri sana. Tulitengeneza ubao wetu wa bao kwa kutumia mchanga na kuchimba mashimo nane tu. Tulitumia kokoto kama mbegu. Nilijifunza kupanga vizuri mbegu na kuhesabu kabla sijapanda. Nilijifunza kuwa na uvumilivu na kuheshimu mwenzangu wakati tunacheza.

Watoto wengi wanapocheza bao, wanajifunza kuhesabu, kujumlisha na kupanga mikakati. Pia wanapata nafasi ya kushirikiana na wenzao kwa amani. Mchezo huu unasaidia pia watoto kuwa wavumilivu wasio na hasira wanaposhindwa. Hili ni jambo zuri kwa tabia ya mtoto anapokua.

Zaidi ya hayo babu alinifundisha kua bao ni njia ya watoto kujifunza kuhusu utamaduni wao. Ni mchezo wa asili unaotambulika Afrika na una historia ndefu. Watoto wanapocheza bao wanatunza urithi wa mababu zao.

Kwa ushauri wa watoto wote wafundishwe mchezo wa bao. Ni mchezo wa kufurahisha, unaofundisha maadili na pia unasaidia maendeleo ya akili. Badala ya kutumia muda mwingi kwenye simu au televisheni watoto waendelee kucheza michezo ya asili kama bao ili wajifunze na kustarehe.


emakulatemsafiri@gmail.com

0654903872


0/Post a Comment/Comments