FAIDA ZA MTOTO KULALA MCHANA

 

Emakulata Msafiri

Watoto wadogo wanahitaji usingizi wa kutosha ili kukua vizuri na kuwa na afya bora. Kulala mchana ni moja ya mambo muhimu kwao. usingizi wa mchana unasaidia kuimarisha ukuaji wa mwili na ubongo. Wakati mtoto analala mwili wake unatengeneza homoni za ukuaji na seli mpyabjambo linalosaidia kukua kwa haraka na kwa afya.

Lakini pia kulala mchana humsaidia mtoto kupumzika baada ya michezo na shughuli nyingi anazofanya asubuhi. Watoto hutumia nguvu nyingi wanapocheza hivyo wanapolala mchana mwili wao unapata nafasi ya kurudi katika hali ya kawaida na kujiandaa kwa shughuli za jioni.

Aidha kulala mchana huimarisha kumbukumbu na uwezo wa kujifunza. Mtoto anayepata usingizi wa mchana anakumbuka vizuri kile alichojifunza na huwa na akili nzuri.

Pia, mtoto anayelala mchana huwa na tabia nzuri na hupunguza hasira au kulia mara kwa mara. Kupumzika vizuri kunasaidia mtoto kuwa na furaha na kushirikiana vizuri na wenzake.

Kwa jumla kulala mchana ni muhimu sana kwa maendeleo ya mtoto. Wazazi wanapaswa kuhimiza watoto wao kulala mchana ili wawe na afya njema akili nzuri na tabia njema.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments