Emakulata Msafiri
Mchezo wa kidalipoo ni mojawapo ya michezo maarufu sana miongoni mwa watoto. Huchezwa kwa makundi na huleta furaha kubwa kwa washiriki. Mchezo huu huchezwa hasa wakati wa mapumziko shuleni au jioni nyumbani baada ya kazi za shule.
Katika mchezo wa Kidalipoo, mtoto mmoja huchaguliwa kuwa "rede" yaani anayewinda. Yeye hukimbiza wenzake huku akijaribu kuwagusa. Anapomgusa mmoja wa huyo naye hugeuka kuwa rede au anatoka nje ya mchezo kulingana na sheria za kikundi. Mchezo huendelea kwa haraka, na watoto hukimbia huku na kule wakipiga kelele za furaha.
Kidalipoo ni mchezo wa kuvutia sana. Unasaidia mwili kuwa na afya kwa sababu unahusisha kukimbia na kuruka. Pia, huimarisha urafiki na mshikamano kati ya watoto kwa sababu wote hushiriki kwa usawa na kufurahia pamoja. Mchezo huu pia hufundisha nidhamu na kufuata sheria.
Kwa ujumla mchezo huu kufurahisha na wa manufaa. Ni vizuri watoto kuucheza kwani unawasaidia kiafya na kijamii. Tukiendeleza michezo ya asili kutakua siyo tu afya bali pia mshikamano na maadili mema miongoni mwa watoto.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872


Post a Comment