FAIDA ZA BABA KATIKA MALEZI YA MTOTO



Na Emakulata Msafiri

Baba ana nafasi kubwa katika malezi ya mtoto. Kwasababu  baba humfundisha mtoto tabia njema na maadili  Kupitia mafunzo haya, mtoto hujifunza kuwa mnyenyekevu na kuheshimu watu wengine.

Baba ni mfano mzuri wa kuigwa. Mtoto anajifunza kutoka kwa baba jinsi ya kuwa na ujasiri bidii, na kuwa mtu mwenye heshima Kwa Watu warika zote wanaomzunguka katika jamii.

Pia baba hutoa usaidizi wa kihisia kwa mtoto. Anamfariji mtoto wakati wa shida na kumtia moyo ashinde changamoto mbalimbali anazokutana nazo


Baba humlinda mtoto na kuhakikisha anaishi salama. Hii humfanya mtoto awe na amani na kujiamini zaidi
 kwasababu Baba atamfatilia Mtoto Kwa kila hatua anayofanya katika mazingira yanayomzunguka.

Kwa hivyo, baba ni muhimu sana katika kukuza mtoto kuwa mtu mzima mwenye tabia njema na mafanikio maishani hivyo basi waking mama pia wanamchango makubwa katika malezi inabidi washirikiane vizuri na Baba kukuza ukuaji mzuri wa mtoto.

 


 

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

 

0/Post a Comment/Comments