Emakulata Msafir
Migogoro ya wazazi ni hali ambapo baba na mama wanashindwa kuelewana mara nyingi wakigombana mbele ya watoto. Hali hii huathiri sana maisha ya watoto nyumbani. Watoto wanaokua katika mazingira ya migogoro hukumbwa na matatizo ya kihisia, kijamii na hata kielimu.Kuna athari nyingine ambazo zinaweza kuwapata watoto,
Watoto hupata msongo wa mawazo, hofu na huzuni. Wengine hujiona hawapendwi au hawana thamani. Hii huathiri afya yao ya akili na huwafanya washindwe kujieleza au kujiamini.
Pili, watoto wanaoishi katika migogoro huweza kuwa wakaidi, wakorofi au wenye tabia za fujo. Baadhi yao huanza kutumia lugha chafu au hata kuiga tabia za ugomvi walizoona nyumbani. Hali hii huwafanya washindwe kuishi vizuri na wenzao au hata walimu shuleni.
Tatu, migogoro huathiri masomo ya watoto. Wakiwa na mawazo mengi au huzuni hushindwa kusoma vizuri au kupata alama nzuri. Baadhi yao hutoroka shule au huacha kabisa.
Kwa ujumla migogoro ya wazazi ina madhara makubwa kwa watoto. Ni wajibu wa wazazi kutafuta suluhisho la matatizo yao kwa amani ili kuwalea watoto katika mazingira yenye upendo, utulivu na maelewano.
emakulatemsafiri@ gmail.com
0653903872
Post a Comment