ASIYE KUBALI KUSHINDWA SI MSHINDANI

Na Emakulata Msafiri

Palikuwa na kijiji kidogo kilichokuwa na familia  moja yenye mtoto aitwaye Juma. Juma alikuwa mtoto mzuri wa sura na mwenye akili nyingi shuleni. Kila mtu kijijini alimpenda lakini tatizo moja kubwa lilikuwa kwamba Juma alikuwa na kiburi sana.

Wazazi wake walijitahidi kumfundisha adabu na jinsi ya kuishi na watu kwa heshima lakini Juma hakutaka kusikia. Kila alipofanya kosa mama yake alipomkanya, Juma alimjibu vibaya. Baba yake alipomweleza jambo Juma alimpuuza na kusema, “Ninajua kila kitu sihitaji kuambiwa!”

Siku moja baba yake alimwambia asiende kucheza mbali kwa sababu mvua ni kubwana mto umefurika maji, Lakini kwa kiburi chake Juma hakutii. Alienda pamoja na marafiki zake kuogelea mtoni.

Wakati wakicheza ghafla maji yaliongezeka na mkondo ukaanza kumvuta. Wenzake walikimbia na kumuacha. Kwa bahati nzuri watu walimwona na kumsaidia lakini alipata majeraha na aliogopa sana.

Aliporudi nyumbani  alikuwa amechoka na mwenye huzuni. Baba na mama yake walimpokea kwa upendo na kumpa matibabu. Baada ya tukio hilo, Juma alitambua makosa yake. Aliona umuhimu wa kusikiliza na kutii wazazi.

 


emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872

 

 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments