AKILI NI SILAHA BORA

 


Emakulata Msafiri

Siku moja Sungura alikuwa akitembea porini akitafuta chakula. Akiwa njiani alikutana na Fisi ambaye alikuwa na njaa kali.

Fisi alimwambia Sungura, “Nimekuwa nikiwaza siku nyingi jinsi ya kukushika. Leo huponyoki!”

Sungura alikuwa mwepesi wa akili akaona lazima atumie ujanja ili aokoke. Akamwambia Fisi, “Nashukuru sana kwa kunitaka leo. Ila kabla hujanila kuna pango lenye hazina kubwa. Kama tukiwahi sasa hivi tutajua siri ya utajiri!”

Fisi akastaajabu. “Hazina? Wapi hiyo?”

Sungura akamwongoza hadi kwenye pango moja kubwa na akasema, “Ingiza kichwa chako ndani ya pango uone vizuri.”

Fisi akaingiza kichwa chake ndani ya pango, na kwa haraka Sungura akachukua jiwe kubwa na kulizingusha hadi likaziba mdomo wa pango, Fisi akiwa bado ndani!

Fisi alijaribu kutoka lakini kichwa chake kilikwama. Akawa anapiga kelele, “Nisaidie, Sungura! Nakuomba!”

Sungura alitabasamu akamjibu, “Mara ya pili usiwadharau wanyama wadogo. Akili ni bora kuliko nguvu!”

Sungura akaondoka kwa furaha akipiga makofi huku akicheka.


emakulatemsafari@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments