Emakulata Msafiri
Kulikua na mtoto mmoja jina lake Chaupele. Alipenda sana kubishana na wakubwa, na hakumwogopa mtu yeyote. Kila alipoambiwa jambo lazima ajibu na kutoa hoja zake hata kama alikuwa anakosea.
Tabia hii ilimchukiza sana mama yake. Mara nyingi alimwonya akimwambia:
"Mwanangu, naomba uache tabia hii ya kubishia wakubwa. Unaleta picha mbaya mtaani na unanitia aibu."
Siku moja Chaupele alinyamaza akasema kwa sauti ya upole:
"Mama sirudii tena. Naahidi nitakuwa mtoto mwema kila mtu atashangaa."
Mama alifurahi sana akamkumbatia mwanae kwa furaha. Alifikiri mwanae kweli amebadilika.
Lakini kumbe Chaupele alikuwa amemdanganya mama yake. Kesho yake aliendelea kubishana na watu kama kawaida. Alibishana na jirani alibishana na marafiki na hata na watu wazima.
Watu mtaani walianza kumchukia na kumuepuka. Hatimaye, Chaupele alibaki mpweke, hana rafiki na mama yake akawa na huzuni kubwa.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment