SIMU YA MAAJABU YA EMMY

Emakulata Msafiri

Palikuwa na msichana mmoja aitwaye Emmy. Alikuwa na miaka 10 na aliishi na mama yake katika kijiji kidogo cha Mlimani. Emmy alipenda kucheza, kusoma vitabu, na kusaidia mama yake shambani.

Siku moja, mjomba wake kutoka mjini alikuja kumtembelea na kumpa zawadi simu mpya ya kisasa!

“Emmy, hii ni simu yako. Ila tumia kwa busara, usiache shule wala kazi zako za nyumbani, sawa?” alionya mjomba wake.

Emmy alifurahi sana. Alianza kuangalia video kila siku, kucheza michezo ya kwenye simu na kuwasiliana na marafiki kwa ujumbe. Kidogo kidogo, alianza kubadilika:

Shuleni alianza kupata alama za chini.

Mama yake alihuzunika. Siku moja alipomwambia:

“Emmy, simu hii imekuwa kama mchawi. Imekunyang’anya furaha yako ya kweli.”Emmy alinyamaza. Alianza kufikiria

Mwili wake unaumwa kwa kukaa muda mrefu bila m niweke azoezi.Macho yake huumwa sana kila anapotazama skrini.

Siku iliyofuata, aliamka mapema, akaweka simu kwenye droo na kwenda kusaidia mama shambani. Aliomba radhi na kuahidi kutumia simu kwa wakati maalum tu kwa kujifunza na kuwasiliana kwa sababu muhimu.

Tangu siku hiyo, Emmy alirudi kuwa msichana mchangamfu, mwenye afya na mwenye furaha

Teknolojia ni nzuri, lakini ikiwa haitatumika kwa kiasi na busara, inaweza kuharibu afya, mahusiano, na maendeleo ya watoto. Watoto wanapaswa kutumia muda wa skrini kwa kiasi na kupata muda wa kucheza, kusoma na kuzungumza na watu halisi.

emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments