MTOTO MSIKIVU KWA WAZAZI WAKE

Emakulata Msafiri

Bella alikuwa msichana mdogo aliyekuwa akiishi na wazazi wake mjini Iringa. Alikuwa anasoma darasa la tano katika shule ya msingi iliyokuwa karibu na nyumbani kwao. Bella alijulikana kwa tabia njema, adabu na utii kwa wazazi wake.

Siku moja mama yake alimwambia, "Bella, leo usichelewe kurudi kutoka shule. Nenda dukani ununue mkate, maziwa na sukari." Bella alisikiliza kwa makini na kusema "Sawa mama, nitafanya hivyo."

Baada ya kutoka shule, alikataa kujiunga na marafiki zake waliomwalika kwenda kuangalia filamu kwenye kibanda cha jirani. Aliwaambia, “Samahani, siwezi kwenda leo. Mama yangu aliniambia nirudi moja kwa moja nyumbani na kwenda dukani.”

Bella alirudi nyumbani, akatoa sare zake, kisha akaenda dukani kama alivyoelekezwa. Alileta vitu vyote alivyotumwa na mama yake bila kusahau chochote.

Mama yake alifurahi sana. Alimkumbatia Bella na kusema, “Wewe ni mtoto mwenye heshima. Mungu atakubariki sana kwa kunisikiliza na kutii.” Baba yake pia alimpongeza na kusema “Watoto kama wewe ndio wanaojenga taifa lenye maadili.”

Kwa sababu ya tabia yake njema Bella aliheshimiwa shuleni nyumbani na hata mtaani. Alikuja kuwa mfano bora kwa watoto wengine mjini.



emakulatemsafiri@gmail.com

0653903872


0/Post a Comment/Comments