Na, Emakulata Msafiri
Siku moja, katika msitu wa kijani kibichi, aliishi tembo mkubwa mwenye roho nzuri aitwaye Tembo Juma. Tembo Juma alikuwa na nguvu nyingi lakini alikuwa mnyenyekevu na mkarimu kwa kila mnyama.
Siku moja alipokuwa akitembea kando ya mto, alimsikia sungura mdogo akilia kwa sauti. Tembo Juma akakaribia kwa upole na kusema, “Habari ndugu yangu Sungura, kwa nini unalia?”
Sungura akasema, “Nilikuwa nikicheza karibu na mto, lakini sasa nimekwama ndani ya shimo na siwezi kutoka.”
Tembo Juma akatabasamu, akanyoosha mkonga wake mrefu, na kumsaidia Sungura kutoka shimoni. Sungura akasema kwa furaha, “Asante sana Tembo Juma! Nitaulipa wema wako siku moja.”
Tembo Juma akacheka kwa upole, “Wewe ni mdogo sana, Sungura. Lakini asante kwa moyo wako wa shukrani.”
Siku chache baadaye, Tembo Juma alikwenda kutembea msituni tena. Ghafla, alinaswa kwenye mtego wa wawindaji! Alijaribu kujitoa kwa nguvu, lakini mtego ulikuwa mgumu sana.
Tembo Juma akapiga kelele, “Naomba msaada!” Wanyama wengi waliogopa kumkaribia, lakini Sungura akakimbia haraka.
Sungura akasema, “Usijali Tembo Juma! Nitakusaidia.” Kwa kutumia meno yake makali, alianza kukata kamba za mtego kidogo kidogo. Ilimchukua muda, lakini hatimaye akamkomboa Tembo Juma.
Tembo Juma akasema kwa mshangao, “Sikuwahi kufikiri kwamba mnyama mdogo kama wewe angenisaidia. Leo nimejifunza kuwa kila mmoja ana uwezo wa kusaidia, haijalishi ukubwa wake.”
Sungura akatabasamu na kusema, “Ukarimu huwa haupimwi kwa nguvu, bali kwa moyo.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment