Emakulata Msafiri
Mtoto anapolelewa na mzazi mmoja hukumbwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri maendeleo yake. Kwanza, hukosa upendo wa mzazi mwingine, jambo linaloweza kusababisha huzuni na msongo wa mawazo.
Pili, mtoto hukosa mfano wa jinsia nyingine, hali inayoweza kuathiri ufahamu wake wa kijinsia na kijamii na kupelekea MDA mwingine mtoto kujitenga na wenzie na kushindwa kushiriki michezo mbalimbali ya kujenga afya ya mwili
Vilevile, mzazi mmoja mara nyingi hupata ugumu wa kifedha jambo linaloweza kuathiri mahitaji muhimu ya mtoto kama elimu na afya. Mtoto pia huweza kujisikia kutengwa au kunyanyapaliwa na jamii. Hali hizi zote huweza kusababisha mtoto kuingia kwenye tabia hatarishi kama ulevi, wizi, au kushuka kitaaluma.
Hata hivyo, kwa msaada wa jamii na jitihada za mzazi, mtoto anaweza kulelewa vizuri na kufanikisha maisha yake. Ni muhimu jamii iwasaidie ili watoto wao wapate malezi bora.
Kulea mtoto ni jukumu kubwa linalohitaji msaada wa pamoja. Watoto wanaolelewa na mzazi mmoja wanahitaji uangalizi maalum ili kuepuka madhara yanayoweza kuwapata.
emakulatemsafiri@gmail.com
0653903872
Post a Comment