FURAHA YA LEO MAJUTO YA KESHO

 


Na, Emakulata Msafiri 

Palikuwa na kijiji kidogo kilichozungukwa na misitu mikubwa na mashamba ya kijani kibichi. Ndani ya kijiji hicho, kuliishi kundi la sisimizi waliokuwa maarufu kwa bidii yao kazini. Kila siku walikuwa wakikusanya chakula kwa ajili ya msimu wa mvua, ambao ulikuwa ukikaribia.

Miongoni mwa sisimizi hao kulikuwa na mmoja aliyejulikana kwa jina la Mkaidi. Tofauti na wengine, Mkaidi hakuwa na hamu ya kufanya kazi. Kila siku alipenda kucheza, kuimba, na kuzunguka huku na kule, akiwacheka wenzake waliokuwa wakifanya kazi kwa bidii.


“Mbona mnahangaika sana? Wacha tufurahie jua na upepo wa leo. Wakati wa mvua ukifika, tutajua la kufanya,” alisema Mkaidi kwa dharau.

Sisimizi wakamkumbusha: “Tunakusanya chakula mapema ili tusihangaike wakati wa mvua. Hatutakuwa na muda wa kutoka kutafuta chochote wakati huo.”

Lakini Mkaidi hakusikiliza. Aliendelea na starehe zake huku wenzake wakijituma bila kuchoka.

Msimu wa mvua ulipowadia, mvua kubwa ilianza kunyesha kila siku. Upepo ulikuwa mkali, na ardhi ikawa tope. Sisimizi waliokuwa wamejiandaa walikaa majumbani mwao, wakila chakula walichokusanya kwa bidii.


Lakini Mkaidi alikuwa na njaa. Hakukuwa na chakula cha kula, na mvua ilimzuia kutoka. Alijutia uvivu wake, akakumbuka maneno ya wenzake – lakini ilikuwa tayari kashachelewa.



emakulatemsafiri@gmail.com 

0653903872

0/Post a Comment/Comments